Home Uncategorized RIO AKIWASHA, AIPONDA MAN UNITED

RIO AKIWASHA, AIPONDA MAN UNITED


MASHABIKI wa Manchester United, juzi waliondoka karibia wote uwanjani wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Burnley.

Wakiwa kwenye Dimba la Old Trafford, United walijikuta wakilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Burnley na beki wao wa zamani, Rio Ferdinad, amesema mabosi wa timu hiyo wanatakiwa kulitazama hilo kwa kuwa ni udhalilishaji.

Zikiwa zimebaki dakika 15, mchezo umalizike nusu ya mashabiki wa United walikuwa wameshatoka uwanjani.

Rio ambaye alikuwa akichambua mchezo huo kwenye Kituo cha BT Sport, amesema kuwa kikosi cha United kimegharimu pauni milioni 600, lakini haoni jambo lolote la maana.

“Ni kama udhalilishaji kuwa hapa na kuona kile ambacho kinatokea kwenye kikosi cha United kwa sasa. “Huwezi kulinda hilo, mashabiki wametoka uwanjani wote dakika ya 85.

“Watu wa juu kwenye kikosi cha United wanatakiwa kulitazama hili kwa jicho lingine.

“Watoto wadogo kwenye shule hawawezi kuvaa jezi ya Manchester United kwa sasa na hawawezi kutamani kwenda Old Trafford,” alisema Rio, nahodha wa zamani wa United.

United kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye ligi hiyo wakiwa na pointi 34 huku kinara Liverpool wakiwa na pointi 64.
SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA