Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA JUMAMOSI…WAMOROCCO WAJIBU TAMBO ZA SIMBA KIBABE…

KUELEKEA MECHI YA JUMAMOSI…WAMOROCCO WAJIBU TAMBO ZA SIMBA KIBABE…

Raja Twitter

Wakati joto la mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika baina ya Mnyama @simbasctanzania dhidi ya Raja Club Athletic likizidi kushika kasi, huko mitandaoni nako mambo ni moto.

Timu ya Raja Club Athletic inaonekana kama vile umewafikia ujumbe wa Klabu ya Simba wa ”Moto ni Ule ule, Kwa Mkapa hatoki Mtu.” huku ujumbe huo ukinogeshwa na picha la kibabe.

Miamba hiyo ya soka Afrika nayo imeposti ujumbe huo wa Simba ukiambatanishwa na kipande cha video kwenye akaunti yao ya kijamii ya twitter ” Habari marafiki wa Simba SC, Kiswahili changu vipi ?,”

Wekundu wa Msimbazi na Raja Club Athletic wanatarajia kukutana Benjamin Mkapa mchezo wa Ligi ya Mabinbgwa Afrika Jumamosi ya Februari 18, 2023.

SOMA NA HII  PERFECT CHIKWENDE WA SIMBA ATAJA TUZO ANAYOITAKA BONGO