Home Uncategorized HAWA HAPA WACHEZAJI PASUA KICHWA KWA ZAHERA WA YANGA

HAWA HAPA WACHEZAJI PASUA KICHWA KWA ZAHERA WA YANGA



Ibrahim Ajibu

Kesho, Mei 30 mkataba wake unamalizika ndani ya Yanga, bado amekuwa pasua kichwa kwa kocha Mwinyi Zahera kutokana na kuvuruga dili lake la kusepa kwenda TP Mazembe na mpaka sasa hajaonana na kocha wake huyo ambaye ndiye alimshauri ajiunge na Mazembe.

Amissi Tambwe

Amekuwa bora mwishoni licha ya kuanza kwa kusuasua majeruhi yamemfanya asiwe bora, mkataba wake nae upo ukingoni kwa sasa ni mchezaji huru na bado haijawekwa bayana kama ataongezewa mkataba mpya na Yanga.

Thaban Kamusoko

Umri pamoja na kushuka kwa uwezo kwa muda kunamfanya Zahera apate kigugumizi kumuweka kwenye orodha ya wachezaji wake wapya ambao atawatumia mwaka ujao kwenye ligi.

Haruna Moshi

Timu yake ya zamani African Lyon imekwenda moja kwa moja daraja la kwanza na mkataba wake unakamilika mwishoni mwa mwezi huu hivyo atakuwa huru kwa sasa.

Mrisho Ngassa

Msimu huu amekuwa kwenye kikosi cha Yanga ambapo alitokea Ndanda FC,Zahera anamtazama kwa nafasi yake huku akipasua kichwa kujua hatma yake.

Ramadhan Kabwili

Mlinda mlango namba moja wa Yanga amekuwa bora msimu huu licha ya kutopewa nafasi mara kwa mara, kesho mkataba wake unakamilika bado hajazungumza na uongozi wa Yanga juu ya hatma yake, mbivu na mbichi zitajulikana kwani anafuatiliwa na timu moja iliyopo Sudan.

SOMA NA HII  MASHUJAA WAPANIA KUONYESHA USHUJAA WAKIPANDA LIGI