Home Habari za michezo KISA ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA AFRIKA KUSINI…BARBARA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HAYA..

KISA ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA AFRIKA KUSINI…BARBARA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AFUNGUKA HAYA..


Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Soka ya Simba Barbara Gonzalez ni kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Bernard Morrison hawezi kuingia ndani ya ardhi ya Afrika Kusini kutokana na kuwa na kizuizi cha kuingia nchini humo.

Morrison kabla ya kujiunga na vilabu vya Yanga na Simba tayari alishawahi kufanya kazi nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates na aliondoka klabuni hapo kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Pamoja na Morrison kutohusika katika mchezo huo wa marudiano hiyo haijashusha hamasa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez baada ya kudai kuwa Morrison atamaliza mchezo kwenye ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Droo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika imetangazwa hapo jana ambapo Klabu ya Soka ya Simba ya nchini Tanzania imepangwa kumenyana na Klabu ya soka ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

Mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya mtoano unatarajiwa kuanza nchini Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo wenyeji Simba wataikaribisha Orlando Pirates Aprili 17, wiki moja baadaye Orlando Pirates watakuwa wenyeji wa Simba katika dimba la Orlando Stadium jijini Johannesburg.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADA YA KUPATA DILI ULAYA...OPPA AFUNGUKA ISHU YA KURUDI ZAKE BONGO..