Home Habari za michezo MECHI DHIDI YA WASAUZI…ONYANGO, KANOUTE ‘OUT’ SIMBA….PABLO AKUNA KICHWA…

MECHI DHIDI YA WASAUZI…ONYANGO, KANOUTE ‘OUT’ SIMBA….PABLO AKUNA KICHWA…


Kocha wa Simba, Pablo Franco inabidi aanze kukuna kichwa mapema juu ya kuziba pengo la beki wake wa kati Joash Onyango ambaye atakosekana kwenye mchezo wa robo fainali unaotarajia kuchezwa Aprili 17 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba imepangiwa kucheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwenye hatua ya robo fainali, Simba ambayo itaanzia nyumbani itamkosa Onyango ambaye ana kadi tatu za njano alizoonyeshwa katika mechi za makundi.

Onyango amepata kadi za njano kwenye mechi dhidi ya US Gendermerie 1-1, Berkane 2-0 Simba na Simba 4-0 US Gendermerie.

Kanoute alipata kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya Berkane na mechi zote mbili za US Gendermarie hivyo atakosekana kwenye mchezo ujao.

SOMA NA HII  BWALYA AZIDI KUNG'AA SIMBA...AKABIDHIWA RASMI MAJUKUMU JOHN BOCCO NDANI YA UWANJA...