Home Habari za michezo KUHUSU MRITHI WA ROBERTINHO ….UONGOZI SIMBA WAJA NA TAMKO HILI LA KIBABE….

KUHUSU MRITHI WA ROBERTINHO ….UONGOZI SIMBA WAJA NA TAMKO HILI LA KIBABE….

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba umevunja ukimya na kueleza sababu ya kutaka kupata Kocha aliyebora ambaye watakuwa nao kwenye mipango ya muda mrefu hali iliyopelekea kushindwa kutangaza mrithi wa Roberto Oliviera (Robertinho) kama walivyowaahidi mashabiki.

Awali Simba walisema wiki iliyopita watamtangaza kocha mkuu pamoja na wa viungo lakini imeshundikana na huku wakiendelea na mchakato wa kuendelea kupitia baadhi ya wasifu za makocha ambao waliopeleka CV hizo.

Makocha wengi wanahusishwa kuja kuchukuwa nafasi ya Robertinho akiwemo Sven Vandenbroeck, Abdelhak Benchikha ambaye alikuwa chaguo la kwanza lakini imeshikana kwa kuwa anahitaji dau kubwa na Fernando Da Cruz.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema hawataki kufanya jambo hilo kwa haraka kwa sababu wanahitaji kufanya maboresho makubwa kwa kuleta mtu ambaye wataenda nao sawa kwenye mipango yao ya muda mrefu.

Amesema wanahitaji kuwa walitulivu katika mchakato huo wa kupata mtu aliyekuwa sahihi ambaye atakuja kwa ajili ya kwenda nao katika njia moja kuhakikisha wanapata kocha bora mwenye vigezo walivyoweka.

“Tumeona kuna makocha wengi wakitajwa akiwemo Benchikha ni kocha mzuri, hakuna sehemu viongozi wa Simba wamemtaja, mchakato umechelewa kwa sababu ya kutohitaji kupata kocha baada ya mechi mbili tunamuondoa.

Kuepukana na hilo tumelazimika kuwa makini katika mchakato huu, mashabiki wanatakiwa kuwa wavumilivu kwa sababu ya huo viongozi kupambana kutafuta mtu sahihi wa kuja kuchukuwa nafasi ya Robertinho,” amesema Ahmed.

Amewandoa hofu mashabiki kuwa timu kwa sasa iko sehemu salama chini ya makocha wao Daniel Cadena na Selema Matola ikiendelea na maandalizi jwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

“Benchi la ufundi na wachezaji wanatambua umuhimu wa kupata ushindi katika mchezo wetu wa Novemba 25, mwaka huu tutaocheza nyumbani kusaka alama tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri katika kundi letu.

Lakini pia kwa upande wa wanasimba tumeongea nao wamekubali kusahau yaliyopita hayana faida na zaidi kutengeneza yaliyopo mbele yetu ili kupata furaha katika mchezo huo,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AWAAMSHIA MASTAA, KISA HIKI HAPA