Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA MOROCCO…TAMU NA CHUNGU KWA TAIFA STARS...

KUELEKEA MECHI YA LEO DHIDI YA MOROCCO…TAMU NA CHUNGU KWA TAIFA STARS HIZI HAPA…

Taifa Stars leo

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo wanakibarua kigumu za kuchanga vema karata zake katika mchezo wa pili wa kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

Stars inashuka leo kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 4:00 usiku kusaka ushindi baada ya kufanikiwa kuvuna ushindi wa bao 1-0 mchezo wa ugenini dhidi ya Niger.

Katika mchezo huo tayari kuna wachezaji wa Stars wamekuwa akitajwa kuwa atakuwa hatari juu ya ni Mbwana Samata ambaye nahodha wa Tanzania na Simon Msuva ambaye amewahi kucheza ligi nchini Morocco katika klabu ya Wydad Casablanca.

Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Starts) Adel Amrouch amesema wanaenda kucheza na timu kubwa na anaimani ya kufanya vizuri leo katika uwanja wa nyumbani.

Amesema anaimani na kikosi alichonacho kuna baadhi ya wachezaji walikuwa majeruhi, kikubwa kilichopo kuangaliq makosa yaliyopo kwa sababu maandalizi tuliyofanya mechi iliyopita tofauti na mechi ya Morocco.

“Mechi ya Niger walijitahidi kutumia wachezaji na vipaji tulivyokuwa nao, tunatumia mfumo kulingana na aina ya wachezqji ambao tuko nao, Hatuwezi kutoa mfumo ambao aina ya wachezaji tuliona itakuwa unawapa mzigo mkubwa.

Hata ukiangalia katika viwango vya soka tunaona jinsi Tanzania ilipo, lakini pia timu ya Taifa hatuna muda mwingi wa kukaa na wachezaji na hali ambayo tunalazimika kujiandaa kulingana na mechi iliyopo mbele yetu.

Tunawaheshimu wapinzani wetu ninaimani na vijana wangu wanauwezo wa kupambana na kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa kesho dhidi ya Morocco,” amesema Adel.

Ameongeza kuwa wana timu nzuri na wachezaji wenye uwezo wa kufanya bao na kutengeneza nafasi, wanaendelea kupambana kuwapa mbinu ili kuweza kutumia nafasi hizo kuzaa mabao.

Naye Mwakilishi wa wachezaji wa Stars, Aishi Manula amesema wanaenda kukutana na timu kubwa na wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kupambani taifa kusaka ushindi.

Amesema ni mechi kubwa na ngumu ambayo itaonyesha ushindi mkubwa kwa sababu ya ukubwa wa wapinzani ambao wanakutana nao leo.

“Wachezaji wakubwa wanapenda kucheza timu kubwa tumejiandaa vizuri kupambana kuska ushindi katika mchezo wetu huo tunakutana na Morocco ambayo ipo kwenye ngazi ya juu,” amesema Manula.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Morocco, Walid Regragui amesema anafurahi kufika Tanzania salama na wako tayari kwa ajili ya kusaka ushindi katika mchezo huo dhidi ya Tanzania utakaochezwa leo.

Amesema wamefanya maandalizi ya mchezo huo kama ilivyo kwa mechi nyingine na wanahitaji kufuzu na kusonga mbele hali itawalazimu kushinda mechi dhidi ya Stars.

“Ili mtu afuzu basi mechi ya leo ni muhimu kuhakikisha wanapata ushindi, tunaenda kucheza mechi kwa umakini mkubwa hatuwezi kuangalia tunacheza na timu ya aina gani.

Tanzania hatuwachukulii kama wako daraja la chini tuna waheshimu na wanajituma sana na ukizingatia wanacheza mbele ya mashabiki wao watapambana kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” amesema Walid.

SOMA NA HII  YANGA YAKAMILISHA USAJILI HUU..."HII NI ZAWADI KWA MASHABIIKI WETU