Home Simba SC KOCHA AS VITA AFUNGUKA ALICHOONGEA NA SIMBA

KOCHA AS VITA AFUNGUKA ALICHOONGEA NA SIMBA


BAADA ya tetesi kuenea kuwa simba imemalizana na kocha mkuu wa DR Congo na AS Vita, Florent Ibenge kuwa kocha wao mkuu, hatimaye kocha huyo ameweka hadharani kuwa hajasaini kuifundisha timu hiyo bali alikutana na Simba kwa ajili ya kuongelea kuhusu maendeleo ya soka.

Ibenge kwa sasa yupo nchini Cameroon akiwa na timu ya Taifa ya Congo ambayo kwa sasa inashiriki michuano ya CHAN.

Akizungumzia lengo la kuonana na Ofisa mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Ibenge amesema: “Ni kweli nilikutana na CEO wa Simba na kufanya nae mazungumzo yalikuwa mengi ya kawaida lakini pia yalihusisha kuhitajika kuifundisha timu hiyo ambapo hayakufanikiwa.

“Lakini ukiachana na maombi hayo ya Simba tuliweza kuongea mambo mengi kuhusu maendeleo ya mpira hasa kwa kuwa sisi ni majirani na tunashirikiana katika vitu vingi,”

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WAANZA KUYAPANGIA BAJETI MABILIONI YA CAF SUPER LEAGUE...BAJANA ATAJWA...