Home Simba SC KIMATAIFA SIMBA QUEENS WAFANYE KWELI

KIMATAIFA SIMBA QUEENS WAFANYE KWELI


 MALENGO ya Simba Queens kuweza kutetea taji la Ligi Kuu ya Wanawake yametimia na sasa wana kazi nyingine ya kuweza kufanya katika kupeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa kwa wakati ujao.


Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Simba Queens kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake na ni mara ya kwanza pia mashindano hayo kufanyika hivyo imani yetu ni kwamba kila mmoja anatambua namna ushindani utakavyokuwa.

Ikumbukwe kwamba wakati wanasepa na taji lao mara ya pili baada ya kuwavua ubingwa mabingwa watetezi JKT Queens msimu huu ilifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa rekodi tamu na inayovutia kwa kila timu.

Kutwaa ubingwa bila kupoteza hilo ni jambo la msingi na hapo pongezi kwa benchi la ufundi, wachezaji pamoja na viongozi wa Simba ambao wanapenda kuona mafanikio ya timu yao.

Ukiweka kando viongozi hata mashabiki nao wanapenda kuona timu ikipata matokeo hivyo kwenye mashindano ya kimataifa tunaamini kwamba mtakuwa na mwendo mzuri.

Mwishoni mwa mwezi huu mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika na maandalizi ya Simba Queens yameonekana kuendelea kupamba moto hivyo hakuna namna jambo la msingi ni kujiandaa vizuri.

Kwa wale wachezaji ambao wamepewa majukumu ya kupeperusha bendera ndani ya timu hiyo basi wasikate tamaa wanapaswa kuonyesha ukubwa wa kuwa ndani ya timu hiyo.

Ukweli ni kwamba jambo pekee ambalo linaweza kuwapa ushindi ni maandalizi mazuri pamoja na kuwa na nidhamu kwenye kazi yao pale watakapokuwa uwanjani.

Tunaona kwamba usajili wao unaendelea ukiwahusisha wachezaji wengi wa kimataifa ambao wanatoka kwenye mataifa mbalimbali hilo ni jema na linapaswa kutazwa kwa umakini hasa kwa kusajili wachezaji bora.

Wale ambao watapata nafasi ya kusajiliwa na Simba Queens watambue kuwa kazi kubwa ni kuweza kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ambayo yanaweza kuwa njia kwao kusonga mbele zaidi ya hapo ambapo wapo kwa sasa.

Ipo wazi kusajili wachezaji kutoka Zimbabwe, Burundi, Kenya na nchi nyingine kunahitaji umakini mkubwa na kila mmoja ambaye atasajiliwa basi awe katika ubora unaohitajika na benchi la ufundi.

SOMA NA HII  BAD NEWS...PETER BANDA NNJE MIEZI MITATU...UJUMBE WAKE HUU HAPA...

Hawa wachezaji wakigeni wakiwa bora wataongeza nguvu kwa wazawa ambao wapo ndani ya kikosi cha Simba ambacho kinahitaji kufanya vizuri kwenye mechi zao za kimataifa.

Kwa kufanya vizuri itakuwa nguvu kwa Watanzania kuweza kuwa imara kwenye ushindani na kupata yale matokeo ambayo yanahitajika.

Kumaliza ligi bila kufungwa kusiwafanye waamini kwamba wapo imara kwani kwenye mpira kila kitu kinawezekana.

Hapo kikubwa ambacho kinahitajika ni kwa kila mmoja kuweza kuongeza nguvu na kufanya kazi yao kwa umakini ndani ya uwanja ili kulinda rekodi yao ambayo wameiweka katika ligi.

Kukamilisha mzunguko wa kwanza na wa pili bila kufungwa ni jambo wanalostahili pongezi hivyo hata huko ambapo watakwenda kufanya kazi zao wanapaswa wawe makini na walinde rekodi yao ambayo wametoka kuiweka ndani ya ligi.