Home Uncategorized NAMUNGO KUSAJILI MAJEMBE 11, YUMO NA FUNDI WA BISAHARA UNITED

NAMUNGO KUSAJILI MAJEMBE 11, YUMO NA FUNDI WA BISAHARA UNITED


UONGOZI wa kikosi cha Namungo FC ya mkoani Mtwara ambayo imepanda daraja msimu huu umesema kuwa umejipanga kuwatangaza wachezaji wake wapya hivi 11 hii karibuni.

Nurdine Barola raia wa Burkina Faso anayeitumikia Biashara United imeelezwa kuwa ni miongoni mwa mapendekezo ya mwalimu Hitimana Thiery ambaye alifanya naye kazi alipokuwa Biashara United huenda akawa sehemu ya watakaotangazwa.

 Ofisa Habari wa Namungo, Kidamba Namlia amesema kuwa mwisho wa ubishi juu ya hatma ya Barola utafahamika hivi karibuni kwani amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi hicho.

“Tumejipanga kutangaza wachezaji ambao tutawatumia msimu huu kwenye ligi baada ya kupanda daraja, ni wachezaji wazuri na wenye uzoefu hivyo hata huyo Barola hatma yake itajulikana, maana mkataba wake na Biashara United umekwisha na anafahamiana na kocha hivyo tusubiri tuone.

“Timu itabaki na wachezaji 18 ambao walipandisha timu huku ikisajili wachezaji 11 ambapo hapo tutakuwa na wageni watano na wa ndani sita, hatutaki wachezaji wa majaribio tunataka wachezaji wa kazi ili tusishuke daraja msimu ujao,” amesema Namlia.

SOMA NA HII  SIMBA KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI