Home Uncategorized SIMBA SASA WAANZA KUMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA MALAYSIA

SIMBA SASA WAANZA KUMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA MALAYSIA


KIPRE Tchetche, nyota wa zamani wa Azam FC anayekipiga Klabu ya Kedah inayoshiriki Ligi Kuu ya Malaysia amewekwa kwenye rada za Simba ilikuongeza nguvu ya Kikosi hicho.

Msimu wa 2011 mpaka 2016 nyota huyo alikipiga ndani ya Azam FC anafamiana vema na nahodha wa Simba John Bocco ambaye kwa wakati huo alikuwa akikipiga ndani ya Azam FC.

Habari zinaeleza kuwa uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na wachezaji wa kimataifa ili kupata huduma zao.

Mshambuliaji huyo anakumbukwa kwa kutumia nguvu nyingi na akili ndani ya Uwanja ambapo msimu wa 2013/14 walitwaa taji la Ligi Kuu Bara bila kupoteza mechi. 


“Tchetche anahitajika ndani ya Simba ila mkwanja wake ni mrefu na anataka mshahara wa dola 8,000 kwa mwezi hapo ndipo tatizo lilipo,”. Ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa kwa sasa hawezi sema chochote mpaka muda wa usajili ukifika.

SOMA NA HII  PAMBA SC YAUNGANA NA MBUNGE MABULA KUPAMBANA NA CORONA KWA VITENDO