Home Uncategorized MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC AINGIA KWENYE RADA ZA YANGA

MTAMBO WA MABAO NDANI YA AZAM FC AINGIA KWENYE RADA ZA YANGA


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Yanga upo kwenye mpango wa kumrejesha kundini mshambuliaji wao wa zamani Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC.

Chirwa kwa sasa ni kinara wa kutupia ndani ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba akiwa amefunga mabao nane sawa na David Molinga wa Yanga.

Wakati wa usajili wa dirisha kubwa msimu huu, Chirwa alikoswakoswa na Yanga kutokana na Kocha wa wakati huo Mwinyi Zahera kugoma kumpokea kutokana na kile alichoeleza kuwa ni mchezaji anayependa fedha.


Yanga ikiwa imecheza mechi 27 ambazo ni sawa na dakika 2,430 imefunga mabao 31 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 78.
SOMA NA HII  VIDEO: MLINDA MLANGO WA YANGA APIGA HESABU KUTIMKIA ULAYA, MECHI YAKE NGUMU HII HAPA