Home Habari za michezo FIFA WATOA ONYO LA MWISHO KWA KENYA…IKIKAIDI ITAKUTANA NA ‘RUNGU LENYE NCHA...

FIFA WATOA ONYO LA MWISHO KWA KENYA…IKIKAIDI ITAKUTANA NA ‘RUNGU LENYE NCHA KALI KICHWANI’….


Shirikisho la soka duniani, FIFA, limeitaka serikali ya Kenya kufuta uamuzi wa kulivunja Shirikisho la Soka la Kenya na kuweka kamati ya muda la sivyo nchi itasitishwa kujihusisha na shughuli zote za soka kwa muda usiojulikana.

Katika barua iliyotumwa kwa katibu mkuu wa shirikisho lililovunjwa Barry Otieno, Fifa iliitaka serikali: “kubatilisha uamuzi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri wa tarehe 11 Novemba 2021 kuteua kamati ya muda badala ya Kamati Tendaji iliyochaguliwa ya FKF.”

Hatua hii imekuja ikiwa ni muda mfupi baada ya Rais wa Fifa Gianni Infantino kutangaza kusimamishwa kwa muda usiojulikana kwa shughuli zote za kandanda wakati wa Mkutano wake na waandishi wa habari.

“Bila ya kuathiri uchunguzi wowote wa mamlaka ya kitaifa au vyombo vingine vya mahakama, Baraza la Fifa pia liliamua kusimamisha Shirikisho la Soka la Kenya na Chama cha Soka cha Zimbabwe mara moja kutokana na kuingiliwa isivyofaa na mtu wa tatu,” Infantino alisema.

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Michezo nchini Kenya, Amina Mohamed, Novemba 11 mwaka jana alivunja Shirikisho la Soka la Kenya lililoongozwa na Nick Mwendwa na kuweka Kamati ya Uangalizi.

Amina alimteua Jaji Mstaafu Aaron Ringera kuongoza kamati ya muda, huku mwanahabari Lindah Oguttu akitawazwa kuwa mkuu wa sekretarieti hiyo.

Katibu Mkuu wa Fifa, Fatma Samoura aliiandikia mamlaka ya Kenya mara mbili baada ya kuvunjwa kwa shirikisho hilo, akiiomba serikali, angalau, kurejesha sekretarieti ya chombo hicho wakati wakiendelea kutafuta suluhu.

SOMA NA HII  SABABU ZA JOB KUWA BENCHI, GAMONDI AFUNGUKA KILA KITU