Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA GEITA….PABLO AUTILIA SHAKA UWANJA WA CCM...

SAA CHACHE KABLA YA KUKIPIGA NA GEITA….PABLO AUTILIA SHAKA UWANJA WA CCM KIRUMBA…AITAJA YANGA…


Licha ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kufanyiwa maboresho katika maeneo mbalimbali likiwemo la kuchezea ‘Pitch’, Kocha wa Simba, Pablo Franco ameonyesha wasiwasi na kueleza kuwa alitarajiwa maboresho makubwa na kuufanya uonekane tofauti na mwanzo lakini upo vilevile.

Uwanja huo ulifungwa tangu Februari 23 mwaka huu kupisha maboresho ikiwemo eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo, huduma ya kwanza na kupaka rangi ambapo unatarajiwa kuanza kutumika kesho kwenye mchezo wa ligi kati ya Geita Gold dhidi ya Simba huku majukwaa yakiwa hayajapakwa rangi kama ilivyokusudiwa.

Kabla ya mkutano wake na wanahabari jana jijini Mwanza kuzungumzia maandalizi ya timu yake, Pablo alifika uwanjani hapo saa 6 mchana akiambatana na Meneja wa habari, Ahmed Ally kukagua eneo la kuchezea.

Amesema hakuna tofauti kubwa sana na mara ya mwisho alipofika kucheza na Ruvu Shooting kwani alitarajia uwe bora zaidi ya hapo kwa ajili ya mchezo wa leo na ule wa nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Yanga Mei 28.

“Uwanja uko kama nilivyoukuta mara ya kwanza nilitaraji utakuwa kwenye hali nzuri lakini bado kuna mazingira si ya kuridhisha sana, siyo mzuri sana mwa mchezo wa kesho {leo} hata wa nusu fainali,” amesema Pablo.

SOMA NA HII  BADO NI SIMBA, YANGA SASA NI KIGOMA UNAAMBIWA SIO POA