Home news ZA NDANI KABISAA….;’MWAISA’ KASEKE KUTUPIWA VIRAGO YANGA…MABOSI WAMCHUNIA ISHU YA MKATABA MPYA…

ZA NDANI KABISAA….;’MWAISA’ KASEKE KUTUPIWA VIRAGO YANGA…MABOSI WAMCHUNIA ISHU YA MKATABA MPYA…


ZA NDAANI kabisa ambazo hazina chembe za shaka yoyote ni juu ya safari inayotarajiwa kumkuta, Deus Kaseke ndani ya Yanga kwa msimu ujao.

Ni kwamba hatma ya kiungo mkongwe wa Yanga Deuse Kaseke italazimika kusubiri mpaka mwisho wa msimu kuangalia kama ataweza kuongezewa mkataba wa kuendelea msimu ujao.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema Kaseke ambaye mkataba wake unafikia tamati mwisho wa msimu bado hakuna uhakika wa moja kwa moja kusalia katika kikosi hicho.

Wasiwasi huo umeongezeka zaidi kufuatia kiungo huyo kupoteza nafasi ya moja kwa moja kuanza katika kikosi cha kwanza cha Kocha Nasreddine Nabi anayemtumia mara chache akitokea benchi.

Inaelezwa Kaseke inabidi afanye maombi sana ili kumlainisha Nabi kwani ni yeye tu kwa sasa aliyeshikilia hatma yake kwa msimu ujao.

Nabi ndiye atakayeamua kubaki au kuondoka kwa Kaseke, huku utitiri wa viungo wa pembeni ukiiweka nafasi ya kiungo huyo wa zamani wa Mbeya City na Singida United kusalia kuwa finyu.

Kwa sasa Yanga ina mawinga 6 akiwamo Kaseke, Farid Mussa, Jesus Moloko, Chico Ushindi, Denis Nkane na Dickson Ambundo wanaotumika kila mara na kuonyesha uwezo mkubwa kikosini.

Taarifa zinasema, Nabi ameweka msimamo wake akisema anataka wasalie viungo watano kati ya waliopo sasa.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO MAZITO...NCHIMBI ATEMANA NA YANGA MAZIMA..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA...