Home Azam FC AZAM FC NA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU

AZAM FC NA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU

Habari za Azam

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, amesema bado kikosi chake kipo kwenye mbio za ubingwa na kwa sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya michezo yao ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo kutoka nchini Senegal amesema katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kujiweka vizuri kuelekea kwenye michezo yao ya ligi kuu.

Dabo amesema licha ya kupoteza mechi huko nyuma, anaamini ligi ni sawa na riadha za mbio ndefu kwa kuwa bado kuna michezo mingi mbele.

Amesema wanahitaji kujiandaa kama wanavyofanya kwa ajili ya kutafuta matokeo katika michezo iliyopo mbele yao kwa kusaka alama tatu katika kila mechi ili kufikia malengo yao.

“Kwa sasa tunaendelea na mazoezi, tutakuwa na mechi ya kirafiki ya kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi yetu na kujiandaa kwa mechi zijazo,” amesema Dabo na kuongeza,

“Bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa kwa sababu kuna mechi nyingi mbele yetu, tunapaswa kufanya vizuri kwenye kila mechi bila kuwaangalia wenzetu wanafanya nini, naamini kama tatafanya vizuri kwenye mechi zetu nafasi ya ubingwa bado tunayo” amesema Dabo.

Aidha, amesema anashukuru kwa sasa kwenye kikosi chake hakuna majeruhi na wachezaji wake wamefanya mazoezi kwa muda wa wiki mmoja na mwishoni mwa wiki hii watakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

“Mchezo huo utazidi kunipa mwanga wa kuona ubora wa kikosi changu na mapungufu ya kufanyia kazi kabla ya mechi yetu ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar,” amesema Dabo.

SOMA NA HII  ISHU YA SIMBA V YANGA KUPIGWA KWA MKAPA IPO HIVI