Home Habari za michezo GUEDE APEWA MECHI MBILI TU YANGA….AKIZINGUA ‘ANAPIGWA CHINI CHAP’ HARAKA…

GUEDE APEWA MECHI MBILI TU YANGA….AKIZINGUA ‘ANAPIGWA CHINI CHAP’ HARAKA…

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amempa mechi mbili mshambuliaji wao mpya, Joseph Guede kwa ajili ya kuimarisha uwezo wake na kuongeza muunganiko na wachezaji wengine.

Gamondi alisema dakika 180 zinatoka kabisa kumfanya mchezaji huyo kukaa vizuri na kuanza kuonyesha alichokuwa nacho akishirikiana na wachezaji wengine.

Guede ni miongoni mwa ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga amesajiliwa kipindi cha dirisha dogo ikiwa lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, akiwemo Shekhan Ibrahim na Augustine Okrah

Mshambuliaji huyo ambaye alitarajiwa kutua nchini juzi lakini alikwamia Morocco kwa sababu ya Visa na leo au kesho anatarajia kufika Tanzania na kujiunga na kikosi cha timu hiyo inayoendela na mazoezi uwanja wa Avic Town, Kigamboni.

Kocha huyo anahitaji kuimarisha uwezo wake pamoja na kuongeza muunganiko pamoja na wachezaji wengine ndani ya kikosi hicho ambacho kinapambana kutetea taji lake la ligi.

Amesema anahitaji kupata muda wa kumuamgalia nyota huyo ambaye amechelewa kuungana na wenzake kwa kumpa mechi na kutengeneza muunganiko na wenzake haraka kabla ya kurejea kwenye mashindano ikiwemo ligi kuu, FA na ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kocha Gamondi anahitaji kumuona Guede katika mechi na ametaka mechi mbili za kutengeneza muunganiko wa kikosi chake, anafanya kwa nyota huyo baada ya wengine wapya kucheza katika kombe la Mapinduzi,” amesema kocha huyo.

Ameongeza kuwa Okrah na Shekhan walionekana katika kombe la Mapinduzi na kocha kufanikiwa kutengeneza muunganiko isipokuwa Guede ambaye kocha (Gamondi) anahitaji kumpa mechi mbili kwa lengo la kuwa sawa na wenzake ili kufikia malengo yao.

Kuhusu mechi za kirafiki, Kocha huyo amesema baada ya kucheza mechi moja ya ndani, hawatakuaa na mchezo wowote wa kirafiki ndani ya wiki hii, leo (Ijumaa) watakuwa na mazoezi jioni na kesho (Jumamosi) saa 3:00 asubuhi.

SOMA NA HII  MANARA ATUPA DONGO HILI JIPYA SIMBA...ADAI KILA 'MBWA' HUMJUA BOSS WAKE...