Home Habari za michezo HAWA WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA NAO SI HABA AISEE…WAPATA ‘KOCHA...

HAWA WAPINZANI WA YANGA LIGI YA MABINGWA NAO SI HABA AISEE…WAPATA ‘KOCHA LA MBINU ZA USHINDI’…ALIKUWA AL HILAL..


Wapinzani wa Yanga kwenye hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika, Zalan FC ya Sudan ya Kusini juzi wamemtambulisha kocha mpya Baping Alliab.

Alliab ambaye amewahi kuwa Kocha wa Al Hilal Wau Sudan Kusini na kubeba Kombe la Ligi ataiongoza Zalan kwenye mechi za Afrika ambapo mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Septemba 9 hadi 11 huku marudiano ikichezwa Septemba 16 mpaka 18.

Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atacheza na mshindi kati ya St.Georges ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

“Uongozi wa Zalan FC unathibitisha kumteua Baping Aliap kama kocha mkuu wa Zalan FC kwa kipindi cha mwaka mmoja (1) ikitegemea kumuongeza mkataba kutokana na kiwango timu itakachoonyesha,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Kocha huyo msimu uliopita alikuwa anakinoa kikosi cha Al Hilal Wau ambapo waliibuka Mabingwa wa Sudan Kusini.

SOMA NA HII  POLISI TZ:- HUYU MORRISON SIO POA KABISA ...WAFUNGUKA ALICHOWAFANYIA UWANJANI...CAF YAHUSISHWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here