Home Habari za michezo AHMED ALLY:- GAMONDI AJE KWENYE MAZOEZI YA SIMBA …HATUNA JAMBO DOGO SISI…

AHMED ALLY:- GAMONDI AJE KWENYE MAZOEZI YA SIMBA …HATUNA JAMBO DOGO SISI…

Habari za Michezo

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamemkaribisha Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Ángel Gamondi kufika Simba Mo Arena kushuhudia mazoezi yao kuelekea mechi yao ya dabi Jumapili Novemba 5, 2023.

Ukaribisho huo umetolewa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally alipokuwa akiuzungumzia mchezo huo leo Oktoba 30, 2023.

“Kikosi kitaingia kambini kesho Jumanne, kwa kawaida mechi za ndani huwa tunaingia siku tatu kabla ya mchezo lakini hii tunawahi. Tumeutolea macho mchezo huu kuhakikisha tunapata ushindi.”

“Kocha wao ameshakuja kwenye mechi tatu hadi sasa na leo tunatangaza kumkaribisha kwenye mazoezi yetu yatakayofanyika Mo Simba Arena. Tunamualika rasmi aje siku yoyote anayotaka.”

“Sisi hatuna jambo dogo hivyo tutafanya hamasa, ni mchezo wetu, tutautangaza tutakavyo tunajua watu watakuja lakini lazima tuichangamshe. Tutakuwa na wiki ya mchakamchaka wa kuaga kwao aage atarudi Jumatatu ya Novemba 6, 2023.”

“Siku ya Ijumaa tutakuwa na biryan la derby. Bado tunaangalia eneo la kufanyia.”- Ahmed Ally.

SOMA NA HII  RASMI..SHIBOUB NA MUAIVORY KUKIWASHA KWENYE MAPINDUZI NA SIMBA...DILI LAO LIMEKAA HIVI....