Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA UBINGWA YANGA….DICKSON JOB AZIDI KUFUNGUKA….AMTAJA MWAMNYETO…

KUHUSU ISHU YA UBINGWA YANGA….DICKSON JOB AZIDI KUFUNGUKA….AMTAJA MWAMNYETO…

Beki wa klabu ya Yanga Dickson Job amesema hayupo tayari kuona timu yake inapoteza kwasasa kwa sababu lengo lao ni kumaliza Ligi bila kufungwa.

Yanga mpaka sasa wamecheza mechi 21 bila kupoteza na kuifanya iwe timu pekee ambayo haijafungwa kwenye Ligi.

Maneno hayo yamesemwa na beki huyo kuwa kikubwa mpaka sasa kwanza atuhitaji kupoteza mchezo wowote na ili tusipoteze tunahitaji kucheza mechi bila
kuruhusu goli kwa kila mchezo huku sisi kama walinzi wa timu tupo tayari kwa ajili ya kupambana ili kutimiza malengo yetu.

”Mimi na Mwamnyeto tuna maelewano makubwa na kucheza kwetu muda mrefu tunajuana vizuri na ndio maana kila mmoja anatoa kile anachostahili kwa wakati.” amesema Job.

Dickson Job amejiunga na Yanga kwenye msimu dirisha dogo la msimu uliopita na tangu ameingia kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi amejihakikishia nafasi akicheza sambamba na Bakari Mwamnyeto. Awali mashabiki wa Yanga walikuwa na wasiwasi na kimo cha Job.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA WAITINGISHA YANGA ...MBRAZILI ALETA MAMBO YA VIPERS ...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here