Home Habari za michezo RAISI WA YANGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU USAJILI WA MSIMU HUU

RAISI WA YANGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU USAJILI WA MSIMU HUU

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa watafanya usajili mdogo msimu huu kwa ajili tu ya kuboresha kikosi chao kuelekea msimu uliopita kwani kikosi chao karibia chote kilichowapa ubingwa misimu miwili mfululizo bado kipo imara.

Hersi amesema hayo leo ikiwa ni saa chache baada ya Kibabage kutangazwa kusajiliwa Yanga akitokea Singida Fountain Gate na tayari ameshaondoka na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kwenda Malawi kwenye mchezo wa kirafiki na Nyasa Big Bullets wakati wa sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Taifa hilo.

“Sisi tumekuwa sio watu wa kelele kelele, sisi tunaenda kwenye yale tunayoyahitaji. Tumesajili wachezaji wazuri ambao watakwenda kutusaidia msimu ujao na usajili huo mtauona, tumeanza na Kibabage na wengine watakuja kulingana na watu wetu wa media walivyopanga.

“Niwatoe hofu Wanayanga, hatuna papara wala sababu ya kupiga kelele, tumechukua ubingwa na mataji yote hapa nchini msimu uliopita, tunakwenda kuongeza ubora kidogo kwenye timu yetu ili tuweze kutetea ubingwa wetu kwa mara ya tatu sasa,” amesema Eng. Hersi.

SOMA NA HII  YANGA YATOA SIRI NZITO USAJILI WA MUSONDA...ULE NI USAJILI WA KIMKAKATI