Home Habar za Usajili Simba SIMBA SC IMEPANIA KURUDISHA UFALME WAKE BAADA YA KUKOSA MATAJI…. LEO KLABU...

SIMBA SC IMEPANIA KURUDISHA UFALME WAKE BAADA YA KUKOSA MATAJI…. LEO KLABU YA SIMBA IMEMTANGAZA MCHEZAJI WAKE HUYU MPYA

Tetesi za Usajili Simba

Baada ya kumtambulisha Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Cameroon Leandre Willy Essomba Onana leo Jumatano (Julai 05) kupitia vyanzo vya habari vya Klabu ya Simba, Meneja wa Habari na Mawasilino wa klabu hiyo Ahmed Ally amefunguka mazito kuhusu mchezaji huyo.

Onana anakuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa Simba SC katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa 2023/24, ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa michuano ya ndani na nje ya Tanzania.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya kijamii kufunguka kuhusu mchezaji huyo, ambaye amesajiliwa Simba SC akitokea Rayon Sports ya Rwanda, ambayo ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya tatu, ikitanguliwa na APR iliyoibuka bingwa wa Ligi hiyo, ikifuatiwa na Kiyovu FC.

Ahmed Ally ameandika: Huu ndo usajili bora tangu dirisha la usajili lifunguliwe msimu huu nchini Tanzania

Mchezaji anatoka Taifa la mpira

Mchezaji amefunga magoli mengi

Mchezaji ana assist nyingi

Mchezaji ana tuzo nyingi

Mchezaji anatokea kulia, kushoto, katikati

Mchezaji huko alikotoka timu pinzani zimeshukuru kuondoka kwake maana alikua anawatesa

Mchezaji bado kijana na ana uwezo mkubwa

Mchezaji ana uwezo wa kuchezea mpira na kupiga mashuti ya mbali

𝐇𝐚𝐩𝐚 𝐭𝐮𝐦𝐞𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐦𝐜𝐡𝐞𝐳𝐚𝐣𝐢

Klabu ya Simba SC imemsajili Leandre Willy Essomba Onana kama mchezaji huru akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kwa Mkataba wa Miaka miwili.

Onana mwenye umri wa Miaka 23 Msimu uliopita alifanikiwa kuwa Mchezaji bora na Mfungaji bora wa Ligi Kuu Nchini Rwanda akifunga magoli 15 na kutoa asisti 10 kwenye Michezo 20 ya Ligi hiyo.

Anasifika kwa kasi, chenga na stamina akiwa na mpira, sifa ambazo zimekuwa zikimuwezesha kuwa kipenzi cha mashabiki wengi wa soka wanaomfuatilia huko nchi kwao Cameroon na hata nchini Rwanda alikotoka, pia anatarajiwa kuwa na wafuasi wengi katika ardhi ya Tanzania pindi tu atakapoanza kuitumikia Simba SC katika michezo ya Michuano ya msimu ujao 2023/24.

Vyanzo vyetu vya uhakika kutoka karibu na Mchezaji huyo vimeeleza kuwa, Simba SC imemsajili nyota huyo kwa dola za kimarekani 200,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Milioni 495 na huku akipokea Mshahara wa shilingi milioni 19 kwa Mwezi.

SOMA NA HII  KAPOMBE AFUNGUKA WALICHOFANYIWA MASTAA WA SIMBA KUELEKEA MECHI NA YANGA KESHO...