Home Habari za michezo MOMO AWASHAURI VIONGOZI WA SIMBA, HERSI WA YANGA ATAJWA

MOMO AWASHAURI VIONGOZI WA SIMBA, HERSI WA YANGA ATAJWA

Habari za Yanga

Mchambuzi kutoka Wasafi Fm Ricardo Momo amewapa ushauri viongozi wa Simba wajifunze kwa Rais wa klabu ya Yanga SC Injinia Hersi Said namna ambavyo anaendesha timu.

Ricardo amesema Hersi ndani ya muda mfupi ameweza kutengeneza historia ndani ya Klabu ya Yanga kwa kufanya mambo mengi muhimu kwa ajili ya Wapenzi na wanachama wao.

Mchambuzi huyo amegusia usajili Bora ambao Hersi uwewawezesha kufika fainali ya kombe la Shirikisho na kufuzu hatua ya makundi ligi ya Mabingwa baada ya miaka 25.

Aidha, Momo amesema Yanga wameweza kumfunga Tano mtani ni jambo kubwa na la kihistoria kwa vilabu hivyo.

“Yanga pia wameweza kuchaguliwa kuwania timu Bora ya mwaka katika tuzo za CAF hiyo inaletwa na Uongozi bora.”

Momo amewashauri na Viongozi wa Simba kUbadili mfumo wao wa kuendesha klabu hili kupata mafanikio zaidi.

SOMA NA HII  MUSONDA:- NITAIBEBA YANGA MABEGANI...TP MAZEMBE NILIWAONYESHA..."MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA