Home news PABLO AANZA KUKIWASHA SIMBA…AJIBU, MKUDE KAMA KAWAIDA YAO…GADIEL MICHAEL MHHH…

PABLO AANZA KUKIWASHA SIMBA…AJIBU, MKUDE KAMA KAWAIDA YAO…GADIEL MICHAEL MHHH…


KOCHA mpya wa Simba, Pablo Franco ameanza kukiangalia kikosi chake kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya akademi ya Cambiasso uliochezwa jana Jumamosi kwenye uwanja wa Boko Veterani.

Pablo katika kipindi cha kwanza aliwapanga Beno Kakolanya,  Yusuph, Gadiel Michael, Pascal Wawa na Abdulsamad Kassim.

Wengine ni Jonas Mkude, Yusuph Mhilu, Hassan Dilunga na Ibrahim Ajibu, kutoka timu B, Jimson Mwanuke.

Simba kwenye mchezo huo walikuwa wakisimamiwa na benchi lote la ufundi ambalo liliongozwa na kocha Pablo.

Pablo aliwataka wachezaji wake wawe watulivu na kucheza mpira wa kuonana muda wote wakisaka bao la kuongoza.

Dakika 20 Simba ilipata bao la kwanza kupitia kwa mchezaji wa timu b akitumia makosa ya kipa wa Cambiasso ambaye alishindwa kuudaka mpira wa juu uliopigwa na Ibrahim Ajibu na mshambuliaji huyo aliumalizia.

Licha ya bao hilo timu ya Cambiasso iliendelea kupambana na kucheza soka safi sawa na walivyokuwa wanacheza Simba.

Beki wa Simba, Gadiel Michael alikuwa anasimamiwa kwa umakini na kocha Pablo Franco ahakikishe anapiga krosi za uhakika zinazoingia ndani ya boksi.

Dakika 41 Simba ilipata bao la pili kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa  na Hassan Dilunga baada ya ya mchezaji wa timu B kufanyiwa madhambi ndani ya boksi.

Dakika 64 Cambiasso walipata bao la kwanza kupitia kwa nahodha wao aliyefyatua shuti kali na kwenda moja kwa moja wavuni huku kipa wa Simba, Jeremiah Kisubi akiwa hajui la kufanya.

Bao hilo liliwaamsha wachezaji wa Cambiasso na kushambulia mara kwa mara na kuongeza presha langoni kwa Simba.

Dakika 68 Cambiasso walisawazisha bao la pili na kuufanya mechi hiyo ikimalizika kwa sare 2-2.

SOMA NA HII  BAADA YA SIKU YA WANANCHI NA SIMBA DAY..MASAU BWIRE AIBUKA NA USIKU WA RUVU SHOOTING