Home news FEI TOTO APEWA NAMBA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA

FEI TOTO APEWA NAMBA NDANI YA KIKOSI CHA SIMBA


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa namna anavyokitazama kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi anakubali uwezo wa nyota wengi ikiwa ni pamoja na Feisal Salum.


Manara amesema kuwa wengi wanaibeza Yanga wakidhani haina wachezaji wazuri jambo ambalo sio kweli kwani kuna wachezaji wazuri ambao wanaweza kupata nafasi ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Didier Gomes.

“Unajua wengi hawajui kwamba Yanga ina wachezaji wazuri ambao wengine kati yao wanaweza kucheza kikosi cha kwanza Simba angalau wakagombania namba ikiwa ni pamoja na Fei Toto.

“Fei Toto anajuhudi na anakipaji ambacho ukiangalia unaona kwamba anaweza kugombania namba Simba. Kugombania namba Simba sio mchezo, napenda namna anavyocheza,” amesema Manara.

Ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2020/21 katika Ligi Kuu Bara, Fei amecheza jumla ya mechi 23 kati ya 27 na kutumia dakika 1,935 na alitupia bao moja mbele ya Mwadui FC.


SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOONGEZA MKATABA MPAKA 2025