Home news MGOMBEA MWINGINE TFF ACHUKUA FOMU LEO

MGOMBEA MWINGINE TFF ACHUKUA FOMU LEO


LAMECK Nyambaya leo Juni 9 amechukua fomu za kugombea nafasi ya Kamati ya Utendaji ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).

Nyambaya ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA).

Aliambatana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya DRFA ambaye ni mchambuzi wa soka, Shaffih Dauda aliyevaa miwani pichani.

Zoezi la utoaji fomu kwa wagombea uongozi TFF lilianza hana Juni 8 ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Agosti 7, 2021.

Fomu kwa wagombea inapatikana kupitia tovuti ya TFF na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Juni 12 saa 10 jioni.

SOMA NA HII  CHAMA AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUTUA KAMBINI UTURUKI, KUHUSU KIMATAIFA FULL MIKWARA