Home Habari za michezo DILI LA MANZOKI KUTUA BONGO NDIO BASI TENA….SIMBA WAZIDIWA UWEZO NA WACHINA….

DILI LA MANZOKI KUTUA BONGO NDIO BASI TENA….SIMBA WAZIDIWA UWEZO NA WACHINA….

Taarifa za uhakika zinaeleza Simba SC wameshindwa kukamilisha dili la Cesar Manzoki kukipiga kwenye klabu yao kutokana na timu yake ya sasa, Dilian kuvutiwa na huduma yake na kuweka Ofa kubwa mezani.

Mabosi wa Dilian tayari wamefanya mazungumzo na Manzoki na kukubaliana kumpa mkataba mwingine wenye thamani kubwa na mshahara ambao ni mrefu zaidi ya ule wa awali.

Inaelezwa mshahara wa Manzoki kwenye mkataba wake mpya huko China anaweza kuvuta zaidi ya Sh60 milioni kwa mwezi kama mshahara na ile hela ya kusaini mkataba ni zaidi ya Simba iliyokuwa tayari kumpatia.

SOMA NA HII  BALOZI WA TANZANIA AKUTANA NA YANGA NIGERIA, KAZI IPO LEO