Home Uncategorized JONAS MKUDE HATAKI MCHEZO NDANI YA SIMBA

JONAS MKUDE HATAKI MCHEZO NDANI YA SIMBA

JONAS Mkude, kiungo wa Simba amesema kuwa kwa sasa anajifua vilivyo ili kulinda kipaji chake alichonacho.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona wachezaji wengi wapo nyumbani baada ya kambi kuvunjwa.

Mkude amesema:”Kwa sasa ninafuata maelekezo niliyopewa na Kocha Mkuu (Sven Vandenbroek) ili kuwa fiti na ninachukua pia tahadhari kuhusu Virusi vya Corona.

“Kocha ametoa program maalumu ambayo ninaifanyia kazi na ni muhimu kufanya hivyo ili kuwa bora kwani mazoezi ni muhimu,” .

Mkude amehusika kwenye mabao manne ambapo amefunga mawili na kutoa pasi mbili huku Simba ikiwa imefunga mabao 63.
SOMA NA HII  WAWA ASHUSHA PRESHA SIMBA, MASHINE ZAREJEA