Home Uncategorized LAUTARO MARTINEZ AZIVURUGA KLABU ZA ENGLAND, LA LIGA

LAUTARO MARTINEZ AZIVURUGA KLABU ZA ENGLAND, LA LIGA


MACHESTER City inayoshiriki Ligi Kuu England iliyo chini ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola ipo tayari kuinasa saini ya nyota anayekipiga ndani ya Inter Milan, Lautaro Martinez msimu huu wa usajili.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Inter Milan amekuwa akizivutia klabu nyingi kubwa duniani ambapo amefunga mabao 16 akicheza kwenye mechi 31 za mashindano yote.
Miongoni mwa klabu nyingine ambazo zinaiwinda saini ya nyota huyo mwenye miaka 22 ni pamoja na Chelsea ambayo nayo inashiriki Ligi Kuu England huku timu kubwa za La Liga ikiwa ni pamoja na Real Madrid na Barcelona.
Makamu wa Rais wa Inter Milan Javier Zanetti amesema kuwa bado nyota huyo atabaki ndani ya klabu hiyo licha ya kwamba ameonyesha anapenda kwenda kucheza ndani ya Barcelona.
SOMA NA HII  KUMEKUCHA YANGA, KAZI BADO INAENDELEA LEO TENA VIPIMO PAMOJA NA DARASA