Home Uncategorized MAJEMBE HAYA YA KAZI NDANI YA AZAM FC KAMILI KUWAVAA YANGA, TAIFA

MAJEMBE HAYA YA KAZI NDANI YA AZAM FC KAMILI KUWAVAA YANGA, TAIFA


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa mshambuliaji wao namba moja, Obrey Chirwa na nahodha wao Agrey Morris wapo tayari kuwavaa Yanga, kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Juni 21, Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi zake 57 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya tatu na pointi zake 55 zote zikiwa zimecheza mechi 29.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa kila kitu kipo vizuri kwa kuwa wanaamini mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa.
“Chirwa alikuwa mgonjwa na Morris alikuwa ana matatizo ya kifamilia, ila kwa sasa wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya yanga na tunaamini watapambana ili kuzipata pointi tatu.
“Utakuwa mchezo mgumu hilo lipo wazi ila wachezaji wapo tayari kuona namna gani wanaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi yetu ambayo ni muhimu kwetu,” amesema.
SOMA NA HII  YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA SIMBA