Home Uncategorized YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA SIMBA

YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA SIMBA

JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wapinzani wao wasifikirie kupata njia ya kutokea kwenye mechi yao ya watani itakayochezwa Machi,8 Uwanja wa Taifa kesho kwani na wao wamejipanga.
Mechi ya kwanza iliyochezwa Januari 4, Uwanja wa Taifa Simba ilikubali kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema: “Wachezaji tumekubaliana kufanya kazi kwenye mechi zetu zote na sio ya Simba tu lazima tukaze ili kutoa burudani na kutimiza majukumu yetu wanaofikiria Simba itapata mteremko wasahau.
“Ushirikiano ndani ya timu ni mkubwa na kwa sasa tumeona ligi ni ngumu nasi lazima tukaze ili kupata matokeo,” amesema.
Abdul ametoa jumla ya pasi nne za mwisho za mabao ndani ya Yanga ambapo uwezo wake mkubwa ni kutumia mguu wa kuli
SOMA NA HII  ISHU YA LIGI KUSIMAMISHWA SIMBA WAIGUSIA, WAICHOKONOA KIANIA KLABU NYINGINE