Home Uncategorized PACHA HIZI ZINASUBIRIWA KWA HAMU LEO KUJIBU TAIFA

PACHA HIZI ZINASUBIRIWA KWA HAMU LEO KUJIBU TAIFA


LEO uwanja wa Taifa, mashabiki wa Yanga watakuwa uwanjani huku wakiwa wamebeba matumaini makubwa kwa nyota wao ambao wanazidi kupambana wakiwa ndani ya uwanja.
Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 24 na kibindoni ina pointi 47 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 26 na pointi zake 68.
Moja ya vitu ambavyo vinasubiriwa kwa shauku kubwa ni ule muunganiko wa wachezaji ndani ya vikosi hivi vya Kariakoo utakavyojibu kutokana na rekodi kuonyesha kwamba wamekuwa kwenye maelewano makubwa.
Kwa upande wa kucheka na nyavu ndani ya Yanga kinara wao ambaye ni David Molinga anatarajiwa kuliongoza jahazi hilo huku kwa Simba Meddie Kagere akipewa nafasi kubwa ya kuongoza jahazi hilo.
Ametupia jumla ya mabao 15 kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni namba moja na msimu uliopita alitupia mabao 23.
Hizi hapa pacha ambazo zinasubiriwa kwa shauku uwanjani kuona namna gani zitajibu:-
Molinga  na Nchimbi
Molinga akiwa ametupia mabao 8, mawili ametengenezewa na Ditram Nchimbi, nyota mzawa ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alisajiliwa kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Polisi Tanzania.
Pacha yao imehusika kwenye jumla ya mabao 10 kati ya 29 ambayo Yanga imefunga. Molinga ametupia mabao nane huku Nchimbi akimpa pasi mbili za mabao na yeye pia ametupia mabao mawili.
Morrison na Abdul
Licha ya kuwa Juma Abdul ni beki amekuwa na jicho lake kwa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambaye amefunga mabao mawili  ndani ya Ligi Kuu Bara mpishi wake mkuu kwenye mabao hayo aliyofunga mbele ya Lipuli na Mbeya City alikuwa ni Juma Abdul na alimimina majalo yake kwa guu lake la kulia.
Adeyum na Banka
Itakumbukwa kuwa mchonganishi mkubwa wa bao la pili lililomuacha mdomo wazi Aish Manula alikuwa ni Adeyum Seleman ambaye alitoa pasi iliyokutana na purukushani za Mohamed Hussein na Mohamed Issa ‘Banka’. Pacha yao inasubiriwa tena leo ili kuona nini kitatokea.
Niyonzima na Tshishimbi
Hawa wote ni viungo  wakiwa katikati ni mafundi wa kutuliza presha na kupeleka mashambulizi kwa wapinzani. Niyonzima ana bao moja ndani ya ligi huku Tshishimbi akiwa na pasi moja ya bao kwenye ligi pacha yao pale kati ni moja ya vitu vinavyosubiriwa.
Simba
Kahata na Kagere
Hawa wamekuwa kwa pamoja muda mrefu ambapo walicheza wote walipokuwa ndani ya Gor Mahia ya Kenya na sasa wapo ndani ya Simba.
Pacha yao imehusika kwenye mabao 30 kati ya 55 yaliyofungwa na Simba. Kahata ametupia mabao manne na kutoa pasi sita za mabao huku Kagere akitupia mabao 15 na kutoa pasi tano za mabao.
Chama na Luis
Licha ya kwamba wote ni viungo wamekuwa na mchango mkubwa kwenye mechi za hivi karibuni ambapo wamehusika kwenye mabao 13 ndani ya Simba. Luis amefunga mabao matatu na ametoa pasi moja ya bao huku Chama akitoa pasi saba na kupachika mabao mawili.Pacha yao inasubiriwa na mashabiki kuona namna gani itajibu.
Bocco na Dilunga
Bocco ambaye ni nahodha wa kikosi cha Simba amekuwa kwenye kazi ya kukiongoza kikosi chake kupata ushindi. Amefunga mabao matatu na ana pasi moja ya bao ambalo lilifungwa na Hassan Dilunga mwenye mabao sita na pasi moja ya bao.
Mkude na Shiboub
Hawa viungo wanaonekana kuwa na maelewano wakiwa ndani ya uwanja. Sharaf Shiboub mwenye pasi tano za mabao na bao moja mguuni katika moja ya pasi yake alimpa Mkude. Kwa pamoja wamekuwa kwenye ubora pale wanapopata nafasi ambapo Mkude amefunga mabao mawili na ana pasi tatu za mabao. Pacha yao inasubiriwa kesho kuona itakuajekuaje.
Msimu uliopita wa 2018/19 usumbufu mkubwa ulikuwa katikati ambapo leo inategewmewa Feisal Salum kuanza katikati kukinukisha na Jonas Mkude wa Simba hawa nao wapo kwenye ushindani mkubwa wakianza leo huenda itatengenezwa pacha kali kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania.

SOMA NA HII  KWELI HII HATARI WATU WANAIJUA SIMBA KULIKO STARS