Home Uncategorized NYOTA WA SIMBA ALIYETIMKIA ASIA ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI NA VIONGOZI

NYOTA WA SIMBA ALIYETIMKIA ASIA ATUMA UJUMBE HUU KWA MASHABIKI NA VIONGOZI


NYOTA wa Simba, Adam Salamba amesema kuwa ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kucheza nje ya nchi na imetimia baada ya kujiunga na timu ya Al Jahra SC iliyopo barani Asia.

Salamba amesema kuwa anaamini kwamba bado ana nafasi ya kupeperusha bendera kitaifa na kimataifa kutokana na umri alionao kwenye soka kwa sasa.

“Bado ni kijana na nina nguvu ya kufanya mengi kwa sasa, shukrani kwa mashabiki, viongozi wa Simba pamoja na Namungo kwa kunipa ruhusa ya kutimkia huku niliko kwangu ni furaha na fursa njema,” amesema.

Salamba amejiunga kwa mkopo kwenye timu hiyo iliyopo nchini Kuwaiti.

SOMA NA HII  VPL: SIMBA 0-1 RUVU SHOOTING