Home Uncategorized WAARABU WA MSUVA WAMTAKA MUDATHIR

WAARABU WA MSUVA WAMTAKA MUDATHIR


Klabu ya Difaa Al Jadid ya Morocco ambayo anaichezea Mtanzania, Simon Msuva ina mpango wa kumsajili kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahaya.

Kiungo huyo ni mmoja kati ya wachezaji ambao walipeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Afcon ambayo Taifa Stars ilitolewa hatua ya awali kabisa.

Hata hivyo, taarifa zilizopo ni kuwa, Waarabu hao wa Morocco wana mpango wa kutaka kumsajili nyota huyo wa Azam baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

Kiungo huyo, Mudathir Yahya, alisema: “Wakati nikiwa kule Misri kwenye michuano ya Afcon, hakuna mtu yeyote aliyenifuata kuhusu dili hilo, lakini kama lipo, nipo tayari kuondoka.”

SOMA NA HII  MEI 31 YANGA INA BALAA ZITO, YAINGIA ANGA ZA LA LIGA