Home Uncategorized HATA NIKIZEEKA LADHA YANGU IKO PALEPALE

HATA NIKIZEEKA LADHA YANGU IKO PALEPALE


Ukiwa unafikiria uzee utakujaje au utaharibu muonekano wako, Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa, hana hofu na hilo kwani anaamini ule usemi usemao; “ng’ombe hazeeki maini” ambapo amesema hata akizeeka bado sauti yake itakuwa na ladha ileile.

Khadija alisema kuwa kitu kikubwa anachojivunia ni sauti nzuri aliyopewa na Mwenyezi Mungu ambayo alikuwa nayo tangu akiwa msichana mdogo mpaka leo haijabadilika na haitaweza kubadilika mpaka anashika mkongojo.

“Yaani naelekea uzeeni lakini sauti yangu iko palepale haijawahi kuharibika na kamwe haitatokea hivyo hata kama nitashika mkongojo nitaimba na watu watainuka kwenye viti vyao na hiyo ndio maana ya kuitwa malkia,” alisema Khadija

SOMA NA HII  UKIMFUATILIA MO DEWJI UPANDE HUU, UTAGUNDUA JAMBO TOFAUTI