Home Uncategorized WAKILI ANAYEMTETEA MALINZI ACHOKA, AJA NA OMBI MAHAKAMANI..

WAKILI ANAYEMTETEA MALINZI ACHOKA, AJA NA OMBI MAHAKAMANI..


Kesi ya utakatishaji fedha pamoja na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu inayomkabili aliyekuwa rais wa shirikisho la soka nchini (TFF) Jamal Malinzi, pamoja na wenzake imeendelea Katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu chini ya hakimu mkazi, Mayra Kasonde.

Ambapo Malinzi ameendelea kutoa utetezi wa kesi inayomkabili huku akiambatanisha na risiti za fedha alizoikopesha TFF pamoja na risiti za malipo ya fedha hizo.

Upande wa mashataka umepinga utetezi huo kwa madai kuwa risiti hizo hazikuwa na mihuri pamoja na jina la mwekaji sahihi na hoja ya kupinga kielelezo hicho kuwa na mashaka kuwa risiti hizo zinaweza kuwa zimetengenezwa.

Ni zaidi ya dakika 180 ambazo Malinzi amezitumia Kizimbani akijitetea ambapo mbali na Malinzi kuonekana kuwa bado ana nguvu za kuendelea na utetezi huo, wakili wake, Richard Rweyongeza, ameomba hairisho kwa mahakama kwani alikuwa amechoka kumuongoza mteja wake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27, mwaka huu.

SOMA NA HII  RASHID MATUMLA KUHAMISHA MAKAZI