Home Uncategorized HIZI PACHA TATU NI BALAA ZILIKUWA ZIMEWAKA KWA KUCHEKA NA NYAVU

HIZI PACHA TATU NI BALAA ZILIKUWA ZIMEWAKA KWA KUCHEKA NA NYAVU

LIGI Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kuna pacha ambazo zilikuwa ni matata uwanjani kwa kucheka na nyavu.

Vinara kwenye pacha hiyo wanatoka Klabu ya Simba ambao muunganiko wao umehusika kwenye jumla ya mabao 30.

Meddie Kagere na John Bocco wamekuwa na moto ambapo kwenye mabao 63 yaliyofungwa na Simba wamehusika kwenye mabao 30. Kagere ametupia mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao huku Bocco akifunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.

Pacha inayowafuata ni ile ya Namungo inayoundwa na Reliants Lusajo na Blaize Bigirimana ikiwa imehusika kwenye mabao 29.

Lusajo ametupia mabao 11 na kutoa pasi tatu za mabao huku Bigirimana akiwa amefunga mabao 10 na pasi tano za mabao


Paul Nonga na Daruwesh Saliboko wa Lipuli wao wamehusika kwenye mabao 23.


Nonga ametupia mabao 11 na pasi nne za mabao huku Saliboko akitupia mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara


SOMA NA HII  MCONGO HUYU MTUPIAJI ANASUBIRI SIMU YA YANGA ATUE MAZIMA