Home Uncategorized MCONGO HUYU MTUPIAJI ANASUBIRI SIMU YA YANGA ATUE MAZIMA

MCONGO HUYU MTUPIAJI ANASUBIRI SIMU YA YANGA ATUE MAZIMA


NYOTA anayewaniwa na Yanga kutoka DR Congo Mpiana Mozizi, amesema kuwa anasubiri simu ya mabosi wa Yanga ili atue Dar es Salaam.

Mshambuliaji huyo anayekipiga Lupopo FC, amekuwa akitajwa kuwa ndani ya rada za Yanga ambao wanahitaji kuongeza makali ya timu hiyo msimu ujao kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.

Mozizi amesema kuwa anasubiri simu ya mabosi wa Yanga ili aweze kukamilisha utaratibu wa kutua ndani ya klabu hiyo.

“Ninasubiri kuona kwamba ninapigiwa simu na mabosi wa Yanga kwani tayari tumefanya mazungumzo ya awali iwapo kila kitu kitakwenda sawa basi nitatua hapo.

“Ndoto yangu ni kuwa kwenye ubora wangu na kufunga mabao mengi iwapo nitatua ndani ya Yanga,”

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hesabu za kuboresha kikosi zipo ila ni mpaka wakati wa usajili ukiwadia.

SOMA NA HII  Vieira?