Home Habari za michezo KUHUSU SAKATA LA FEI TOTO….MWAMBUSI ‘AIFYTUKIA’ YANGA….AWAPA ‘MAKAVU LIVE’….

KUHUSU SAKATA LA FEI TOTO….MWAMBUSI ‘AIFYTUKIA’ YANGA….AWAPA ‘MAKAVU LIVE’….

Habari za Yanga SC

Aliekuwa Kocha wa Yanga Juma Mwambusi ameisihi Klabu hiyo kumuachia kwa moyo mkunjufu Kiungo wao Feisal Salum ambae yupo kwenye mgogoro na Klabu hiyo akitaka kuvunja Mkataba.

Akizungumza Mwambusi amewataka Yanga kumruhusu Feisal ili akacheze mpira hasa baada ya kukaa muda mrefu pasipo kuonekana Uwanjani.

“Yanga wamuachie tu kijana aondoke. Busara inabidi itumike maana yanga wanafanya vizuri hata bila ya Feisal wamuachie aondoke waokoe kipaji chake maana hata taifa linanufaika na kipaji chake”

“Busara itumike, sawa sheria zipo lakini manufaa ni kwa mtoto, maana anakaa bila kucheza anaharibu kipaji chake, viongozi wa Yanga wafikirie mara tatu, waweke jambo hili likae sawa maana taifa linamtegemea Feisal”

Feisal mara kadhaa amegonga mwamba katika harakati zake za kutaka kuvunja Mkataba na Yanga.

SOMA NA HII  IKIWA USIKU WA ULAYA NI LEO...HAKIKISHA UNAKAMATA ODDS ZA KUSHIBA KUTOKA MERDIANBET...