Home Uncategorized BAKARI MWAMNYETO ATAJA VIPAUMBELE VYAKE ILI ASAINI

BAKARI MWAMNYETO ATAJA VIPAUMBELE VYAKE ILI ASAINI


BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Klabu ya Coastal Union jina lake limekuwa likileta vurugu kwenye upande wa usajili ambapo inaelezwa kuwa msimu ujao atakipiga ndani ya Klabu ya Simba.

Habari zinaeleza kuwa dili lake la kuibukia ndani ya Yanga lilibuma baada ya beki huyo kuhitaji kupewa milioni 100 ili amwage saini ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani.

Mwamnyeto amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo safu yake ya ulinzi ni miongoni mwa zile zinazofanya vizuri ambapo imeruhusu mabao 19 kwenye mechi 28 za Ligi Kuu Bara.

Mbali na kuwa beki pia ana bao moja kibindoni kati ya 27 yaliyofungwa na safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo yenye ngome yake Tanga.

Mwamnyeto amesema:”Kikubwa ninachokitazama ni maslahi yangu pamoja na nafasi ya kucheza ndani ya timu sichagui kambi popote ninacheza.”

SOMA NA HII  KMC YAPOTEZA KWA KUFUNGWA BAO 1-0 MBELE YA KAGERA SUGAR