Home Uncategorized SHEVA: MUNGU AMETENDA MAAJABU NIPO KAMILI GADO

SHEVA: MUNGU AMETENDA MAAJABU NIPO KAMILI GADO


MIRAJ Athuman, ‘Sheva’ kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa ametenda maajabu kwa sasa yupo fiti.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sheva amesema kuwa kwa sasa ameanza mazoezi binafsi pamoja na yale ya pamoja akiwa na wenzake jambo linalompa matumaini ya kuwa bora zaidi.

“Nipo vema ninamshukuru Mungu kwa kuwa tayari nimeanza mazoezi na wenzangu pamoja na yale binafsi jambo ambalo linanipa matumaini ya kuwa bora,” amesema.

Sheva ametumia dakika 508 uwanjani kwenye mechi za Ligi Kuu Bara amefunga mabao sita na kutoa pasi moja ya bao iliyokutana na guu la kulia la Meddie Kagere alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na jeraha la funda la mguu.

SOMA NA HII  ENG HERSI AMPA NENO HILI GSM BAADA YA YANGA KUCHUKUA POINT TATU KIBABE