Home Uncategorized NAHODHA WA WATFORD AGOMEA KUREJEA KAMBINI, WATATU WAKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA

NAHODHA WA WATFORD AGOMEA KUREJEA KAMBINI, WATATU WAKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA


NAHODHA wa Klabu ya Watford, Troy Deeney amesema kuwa hataripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo kutokana na hofu ya maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaitikisa dunia.

Wachezaji wengi wa Watford pamoja na viongozi wa klabu hiyo imeripotiwa kuwa wamegomea kurejea rasmi kambini kuanza mazoezi ya pamoja.

Imeripotiwa kuwa wachezaji watatu wa Watford wamekutwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo ikiwa ni maandalizi ya kurejea kwa Ligi Kuu England.


Ripoti zinaeleza kuwa wachezaji wengi wamejiunga na Deeney baada ya kuweka bayana mpango huo huku wale ambao wamekutwa na maambukizi wakitwengwa kwa muda wa siku saba.

SOMA NA HII  BEKI MKONGWE WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL APATA PIGO