Home Uncategorized HASSAN KESSY APIGA HESABU ZA KUTIMKA NKANA MSIMU UJAO

HASSAN KESSY APIGA HESABU ZA KUTIMKA NKANA MSIMU UJAO


HASSAN Kessy, beki wa pembeni wa Klabu ya Nkana Rangers ya Zambia amesema kuwa anapiga hesabu za kutimka kikosini hapo msimu ujao.

Nyota huyo anayeperusha bendera ya Bongo nje ya nchi alibukia ndani ya klabu hiyo akitokea timu ya Yanga.


Kessy amesema ana ofa zaidi ya mbili na moja ni ya Tanzania ambayo amegoma kuiweka wazi kwa sasa.


 “Mimi ninaruhusiwa hivi sasa kufanya mazungumzo na klabu nyingine ikiwa itanihitaji kwani mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu hivyo mambo yakijibu nitaondoka ndani ya Nkana.”

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA KAGERA SUGAR UWANJA WA TAIFA