Home news WAKATI WAKIWA WANASHINDA KWA TABU..MORRISON AKOLEZA ‘SHIDA’ SIMBA..AFUNGUKA A-Z…

WAKATI WAKIWA WANASHINDA KWA TABU..MORRISON AKOLEZA ‘SHIDA’ SIMBA..AFUNGUKA A-Z…


KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, amefunguka kuwa licha ya hali ngumu wanayokutana nayo mwanzoni mwa msimu huu, bado kikosi hicho kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba, Jumatano iliyopita wakiwa katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo, na kufikisha pointi 11 katika nafasi ya pili nyuma ya Yanga wenye pointi 15, michezo sawa.

Akizungumza na  Gazeti la Championi Ijumaa, Morrison alisema: “Ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu

iliyopita msimu huu kulinganisha na wapinzani wetu, lakini niwahakikishie kuwa bado tuna muda wa kubadilisha hili na kama wachezaji tunafanya kila jitihada kuhakikisha tunapambana kutetea kombe letu msimu huu licha ya upinzani mkubwa ambao tunatarajia kukutana nao kutoka kwa wapinzani wetu.”

SOMA NA HII  GOLI LA 'KIDEO' LA MAYELE LAWAPA MASTAA YANGA MAMILIONI....NABI KAMA KAWA ATOA LAWAMA KWA MTU...