Home Habari za michezo KISA USAJILI WA OKRAH ….ALLY KAMWE KAIBUKA NA HILI JIPYA TENA YANGA…

KISA USAJILI WA OKRAH ….ALLY KAMWE KAIBUKA NA HILI JIPYA TENA YANGA…

Habari za Yanga LEO

Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa usajili ambao wanafanya kwenye timu hiyo ni wa akili kubwa ukiwa na malengo ya kuongeza uimara kwenye timu hiyo.

Young Africans chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Desemba 31, 2023 walifunga kwa utambulisho wa Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ kutoka nchini Ghana Augustino Okra, ikiwa ni zawadi ya funga mwaka.

Ipo wazi kwamba Young Africans ina kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara, inashiriki Kombe la Mapinduzi 2024, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikiwa hatua ya Makundi na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema kuwa wanatambua kwamba mashabiki wanapenda kupata burudanií kutoka kwa wachezaji na kuona kitakachofanyika kwenye usajili.

“Akili kubwa inatumika kwenye kila idara namna ya usajili wa wachezaji pamoja na kuwatambulisha yote haya tunatoa somo kwa wengine na tunaamini watajifunza mengi zaidi kutoka kwetu.

“Benchi la ufundi linatambua kwamba ambacho kinahitajika ni matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza, hilo lipo wazi ndio maana wachezaji wanajituma kutafuta matokeo mazuri kwenye mechi zetu zote” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  KISA KOSA KOSA ZA KIBU DENIS NA KISINDA....CHIRWA AWACHANA MASTAA WA SIMBA NA YANGA...