Home Habari za michezo SHABIKI SIMBA:- ILI KESHO TUSHINDE….WACHEZAJI WAPEWE iPhone 15 na MIL 100 KILA...

SHABIKI SIMBA:- ILI KESHO TUSHINDE….WACHEZAJI WAPEWE iPhone 15 na MIL 100 KILA MMOJA…

Habari za Simba leo

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome Mapovu amesema kuwa ili timu yao ishinde mbele ya Jwaneng Galaxy, mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji anapaswa ajitokeze na kutangaza bosani kubwa kwa wachezaji.

Mchome amesema kuwa, Yanga wamefanikiwa kufuzu wakiwa na mchezo mmoja mkononi kwa sababu ya ubora wa kikosi, hamasa ya idara ya habari ya klabu hiyo ulioleta mwitikio wa mashabiki pamoja na bonasi kubwa ambazo wachezaji hao wanapewa.

Simba atakuwa na kibarua kigumu mbele ya Jwaneng ya Botswana wakiwania kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika, mchezo utakaopigwa jumamosi Februari 3, 2024 katika Dimba la Mkapa.

“Ili Simba iweze kumtoa Jwaneng galaxy, Mo Dewji ajitokeze awape wachezaji iPhone 15 mpya kila mmoja, bajaji za Mo kila mchezaji, free Wi-Fi kila mchezaji na familia yake na bonasi ya Tsh milioni 100 kila mchezaji, watafia uwanjani pale, lakini wakibana mifuko Simba hatutoki.

“Yanga ametoboa kwenye kundi la kifo mbele ya CR Belouizdad kwa sababu wachezaji wanajituma. Wachezaji wa Jwaneng wengi ni vijana, wanajituma sana na wana kiu na mafanikio kuliko wachezaji wa Simba. Galaxy anaweza kutuua tena kwa Mkapa. Mpira sio maneno, mpira ni pesa,” amesema Mchome.

SOMA NA HII  UMESIKIA MDAU ....HILI LA Infinix NA ZUCHU SIO LA KUKOSA MTU WANGU...NI KWA MGUSO WA NOTE 12 VIP TU ...?