Home Habari za michezo KISA KOSA KOSA ZA KIBU DENIS NA KISINDA….CHIRWA AWACHANA MASTAA WA SIMBA...

KISA KOSA KOSA ZA KIBU DENIS NA KISINDA….CHIRWA AWACHANA MASTAA WA SIMBA NA YANGA…

Habari za Simba , Habari za Yanga

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Obrey Chirwa amesema kuna wachezaji Simba na Yanga hawastahili kuvaa jezi za timu hizo kutokana na viwango duni walivyonavyo na timu hizo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuiwalisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

Simba inaiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wakati watani zao Yanga wanawakilisha Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.

Kwa siku za hivi karibuni , baadhi ya mastaa wa timu hizo wamekuwa wakikosolewa vikali na mashabiki zao, ambapo mathalani Simba wamekuwa wakiimba na kukosa umakini kwa Kibu Denis, huku Yanga wakilia na Tuisila Kisinda.

Chirwa alisema Simba, Yanga ni timu kubwa na kila mchezaji anatamani kuzitumikia lakini kuna baadhi ya wachezaji wapo kwenye timu hizo hawana uwezo mzuri na mkubwa wa kuzisaidia mfano ni Tuisila Kisinda na wengine wengi sitaki kuwaweka wazi.

“Sio muhimu sana kuorodhesha majina ya wachezaji hao kwasabau ni kujitengenezea chuki kitu ambacho sio kizuri lakini napenda kuweka wazi kuwa wachezaji waliopata nafasi ya kucheza au hata kukaa benchi wanatakiwa kujitafakari na kujipima kama wanastahili,” alisema na kuongeza;

“Jezi za timu hizo ni nzito zinahitaji heshima na ubora wa hali ya juu ni wazi kuwa kila mchezaji anatamani kuzivaa lakini hadi umepata nafasi hutakiwi kuishia kukaa benchi au kucheza huku ukiwa hauna madhara kwa timu pinzani.”

Alisema wachezaji wengi waliopo Simba na Yanga ambayo sasa inahitaji ubora na ufundi kutoka kwa mastaa wake hawana uwezo na hawastahili kutumikia timu hizo kwasababu wengi wamekuwa wakikaa benchi na hawaonyeshi kama wataweza kucheza na kuisaidia timu.

SOMA NA HII  MIFUMO MITATU ITAKAYOIBEBA YANGA,GOMES ASHUSHA MBADALA WA CHAMA,NI CHAMPIONI JUMATANO