Home Habari za michezo HII HAPA SABABU YA MUSONDA KUCHOMOLEWA YANGA….ISHU NI YAKE NA GAMONDI TU…..

HII HAPA SABABU YA MUSONDA KUCHOMOLEWA YANGA….ISHU NI YAKE NA GAMONDI TU…..

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa licha ya kumpanga mshambuliaji wake kennedy Musonda kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons, kocha huyo alilazimika kumchomoa kabla ya mchezo huo kuanza kutokana na kupata ugonjwa wa red eyes.

Musonda alikuwa kwenye ‘line up’ ya wachezaji waliopaswa kuanza kwenye mchezo huo lakini baada ya kupata ugonjwa huo, nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Farid Mussa.

“Ni kweli nilimpanga Kennedy Musonda aanze kwenye mchezo wa leo na alikuwa tayari kwa ajili ya mechi, ila baadae ikagundulika amepata tatizo la Macho (Red Eyes) ambayo ilimpelekea kupanda kwa homa.

“Sikuwa na namna nyingine zaidi ya kufanya mabadiliko ya haraka na kumpa nafasi Farid Mussa ambaye pia ametusaidia kwenye ushindi wetu wa leo“ amesema Miguel Gamondi.

Hata hivyo, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika Dimba la Sokoine Mbeya na kuendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na alama 40 katika michezo 15 waliocheza na kumaliza raundi ya kwanza ya ligi.

SOMA NA HII  BAADA YA UKIMYA MWINGI ONYANGO AFUNGUKA HAYA