Home news KAULI YA KIGOGO WA SIMBA YAWATIA NDIMU YANGA…WAAMUA KUCHUKUA HATUA NZITO…

KAULI YA KIGOGO WA SIMBA YAWATIA NDIMU YANGA…WAAMUA KUCHUKUA HATUA NZITO…


Yanga imeanza kambi ya siku 9 za kimkakati jana kujiandaa na mechi ya dabi, huku watani zao Simba wakikebehi. Simba na Yanga zitakutana kwa mara ya kwanza msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania bara kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Simba ikiwa mwenyeji na mshindi ndiye atakalia usukani wa Ligi.

Mpaka sasa Yanga inaongoza ikiwa na pointi 19, Simba yenyewe ina pointi 17 na jana imeondoka nchini kuelekea Zambia kwenye mchezo wa marudiano na Red Arrows wa kombe la Shirikisho Afrika, ikiwa na mtaji wa mabao 3-0 iliyovuna nyumbani Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alisema; “Sio washindani wetu wale, Simba ni levo nyingine ndiyo sababu tuko kimataifa, ila tutacheza nao Yanga kwa kuwa nao wanashiriki Ligi tu, ila ni mechi ya kawaida kama zilivyo mechi nyingine ndogo ndogo tunazocheza.”

Alisema baada ya mechi ya Jumapili na Red Arrows, ndipo wataifikiria mechi hiyo na hawataki kuwapa presha wachezaji wao kwa kuwa ni mechi ya kawaida kwao.

Wakati Simba ikiutaja mchezo huo kuwa wa kawaida, jana Yanga imeanza kambi ya kimkakati ya siku tisa kujiandaa na mchezo huo wa dabi ambao msimu huu utakuwa na msisimko zaidi kutokana na ubora wa kikosi hicho kulinganisha na misimu kadhaa iliyopita.

 Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema kuwa wameingia kambini jana kujiandaa na mechi hiyo akisisitiza si kutaka ushindi tu Desemba 11, bali hawatarajii kushuka kwenye msimamo hadi wanachukua ubingwa msimu huu.

“Tutawafunga na ubingwa tutachukua tena kwa kishindo,” alisema Mfikirwa jana.

SOMA NA HII  HUKO OLD TRAFFORD NI FEDHEA MAN U WATANDIKWA VIKALI