Home Habari za michezo TETESI ZA USAJILI ULAYA:- BARCA WAMALIZANA NA INIGO…..

TETESI ZA USAJILI ULAYA:- BARCA WAMALIZANA NA INIGO…..

Tetesi za Usajili Ulaya

MABINGWA wa Hispania klabu ya Barcelona ‘La Blaugrana’ imethibitisha kwamba Inigo Martinez atajiunga na timu hiyo kwa uhamisho huru akitokea Athletic Club.

Kwa muda mrefu La Blaugrana imekuwa ikihusishwa na beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 ambaye amecheza mechi 357 za La Liga akiwa Athletic na wapinzani wa eneo la Basque Real Sociedad.

 

Tovuti ya michezo 90min imesema Martinez amekubali kwenda kukipiga Barcelona na wakati wowote atasaini mkataba wa miaka miwili.

“Taarifa kutoka klabu ya Barcelona imesema : Makubaliano yamefikiwa kati ya FC Barcelona na Inigo Martinez kwa ajili ya mchezaji huyu kujiunga na klabu yetu baada ya mkataba wake na Athletic Club kumalizika.”

Martinez atakuwa mchezaji wa pili kusajliwa Barcelona katika dirisha hili la majira ya joto baada ya Ilkay Gundogan kumwaga wino akitokea Manchester City.

SOMA NA HII  GALLAS: ARTETA HAKUWA TAYARI KUINOA ARSENAL

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here